Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo ya Walawi 8:14-17
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 14 Kisha akamleta ng’ombe dume wa dhabihu ya dhambi, Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha ng’ombe dume huyo wa dhabihu ya dhambi.+ 15 Musa akamchinja, akachukua damu yake+ kwa kidole chake na kuzipaka pembe zote za madhabahu, akaitakasa madhabahu kutokana na dhambi, lakini damu iliyobaki aliimwaga kwenye msingi wa madhabahu, ili aitakase na kutoa juu yake dhabihu ya kufunika dhambi. 16 Kisha Musa akachukua mafuta yote yaliyofunika matumbo, mafuta yaliyo juu ya ini, na figo mbili pamoja na mafuta yake, akateketeza vitu hivyo juu ya madhabahu ili vifuke moshi.+ 17 Kisha akachukua sehemu zilizobaki za ng’ombe dume huyo, ngozi yake, nyama yake, na mavi yake, akateketeza sehemu hizo nje ya kambi,+ kama Yehova alivyomwamuru Musa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki