23 “‘Utakapomaliza kuitakasa kutokana na dhambi, utatoa ng’ombe dume mchanga wa kundi ambaye hana kasoro na kondoo dume wa kundi ambaye hana kasoro. 24 Nawe utawaleta kwa Yehova, na makuhani watawanyunyizia chumvi+ na kuwatoa kwa Yehova wakiwa dhabihu nzima ya kuteketezwa.