-
Kutoka 26:32Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
32 Utalining’iniza kwenye nguzo nne za mshita zilizofunikwa kwa dhahabu. Kulabu zake zitakuwa za dhahabu. Nguzo hizo zitakaa juu ya vikalio vinne vya fedha.
-
-
Kutoka 26:37Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
37 Utatengeneza nguzo tano za mshita na kuzifunika kwa dhahabu kwa ajili ya pazia hilo. Kulabu zake zitakuwa za dhahabu, nawe utazitengenezea vikalio vitano vya shaba.
-
-
Kutoka 36:37, 38Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
37 Halafu akatengeneza pazia la mlango wa hema kwa nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, kitambaa cha rangi nyekundu, na kitani bora kilichosokotwa na kufumwa,+ 38 na pia nguzo zake tano na vibanio vyake. Akafunika kwa dhahabu sehemu ya juu ya nguzo hizo pamoja na kulabu* zake, lakini vikalio vyake vitano vilikuwa vya shaba.
-