42 Baadhi ya watu wa kabila la Simeoni, wanaume 500, walienda kwenye Mlima Seiri+ wakiwa na Pelatia, Nearia, Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi ambao waliwaongoza. 43 Kisha wakawaangamiza Waamaleki+ waliobaki ambao walikuwa wametoroka, nao wamekuwa wakiishi huko mpaka leo.