-
Mambo ya Walawi 11:4-8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 “‘Lakini hampaswi kuwala wanyama wafuatao wanaocheua au wenye kwato zilizogawanyika: msimle ngamia kwa sababu anacheua lakini kwato zake hazijagawanyika. Yeye si safi kwenu.+ 5 Pia, msimle wibari+ kwa sababu anacheua lakini kwato zake hazijagawanyika. Yeye si safi kwenu. 6 Pia, msimle sungura kwa sababu anacheua lakini kwato zake hazijagawanyika. Yeye si safi kwenu. 7 Pia, msimle nguruwe+ kwa sababu ana kwato zilizopasuka na kugawanyika lakini hacheui. Yeye si safi kwenu. 8 Msile kamwe nyama yao wala kugusa mizoga yao. Hao si safi kwenu.+
-