11 Wakaaji wa Yabeshi-gileadi+ waliposikia mambo ambayo Wafilisti walikuwa wamemtendea Sauli, 12 mashujaa wote wakaondoka na kusafiri usiku kucha, wakaondoa maiti za Sauli na wanawe kutoka kwenye ukuta wa Beth-shani. Wakarudi Yabeshi na kuzichoma moto huko.