-
1 Samweli 11:9-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Kwa hiyo wakawaambia wajumbe waliokuwa wamekuja: “Hivi ndivyo mnavyopaswa kuwaambia watu wa Yabeshi kule Gileadi, ‘Kesho wakati wa jua kali mtaokolewa.’” Basi wale wajumbe wakaja na kuwaambia watu wa Yabeshi, nao wakashangilia sana. 10 Ndipo watu wa Yabeshi wakasema: “Kesho tutajisalimisha kwenu, nanyi mtatutendea mpendavyo.”+
11 Siku iliyofuata, Sauli aliwagawa watu katika vikosi vitatu, nao wakaingia katikati ya kambi wakati wa kesha la alfajiri* na kuwaua Waamoni+ mpaka jua lilipokuwa kali. Watu waliookoka walitawanywa hivi kwamba hakuna watu wawili waliobaki pamoja.
-