-
1 Samweli 27:11, 12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
11 Daudi hakumwacha hai mwanamume au mwanamke yeyote ili wasiletwe Gathi, kwa kuwa alisema: “Wasije wakawaambia habari zetu wakisema, ‘Hivi ndivyo Daudi alivyofanya.’” (Alizoea kufanya hivyo muda wote alioishi katika eneo la mashambani la Wafilisti.) 12 Kwa hiyo Akishi akamwamini Daudi akisema moyoni mwake: “Bila shaka ananuka miongoni mwa watu wake wa Israeli, kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu sikuzote.”
-