-
1 Mambo ya Nyakati 10:1-5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Sasa Wafilisti walikuwa wakipigana na Waisraeli. Na wanaume wa Israeli wakawakimbia Wafilisti, na wengi wakauawa kwenye Mlima Gilboa.+ 2 Wafilisti wakamkaribia sana Sauli na wanawe, nao wakamuua Yonathani, Abinadabu, na Malki-shua,+ wana wa Sauli. 3 Vita vikawa vikali sana dhidi ya Sauli, na wapiga mishale wakampata na kumjeruhi.+ 4 Ndipo Sauli akamwambia mtu aliyembebea silaha: “Chomoa upanga wako unichome nao, ili watu hawa wasiotahiriwa wasije kunitendea kikatili.”*+ Lakini mtu aliyembebea silaha hakutaka kufanya hivyo, kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akachukua upanga na kuuangukia.+ 5 Mtu aliyembebea silaha alipoona kwamba Sauli amekufa, yeye pia akauangukia upanga wake mwenyewe na kufa.
-