-
2 Samweli 12:15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Kisha Nathani akaenda nyumbani kwake.
Basi Yehova akamletea pigo mtoto ambaye mke wa Uria alikuwa amemzalia Daudi, akawa mgonjwa.
-
-
2 Samweli 12:19Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Daudi alipowaona watumishi wake wakinong’onezeana, alitambua kwamba yule mtoto amekufa. Daudi akawauliza: “Mtoto amekufa?” Wakajibu: “Amekufa.”
-
-
2 Samweli 13:10-15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Kisha Amnoni akamwambia Tamari: “Niletee chakula* katika chumba cha kulala, ili nikichukue kutoka mkononi mwako na kukila.” Basi Tamari akachukua keki zenye umbo la moyo ambazo alikuwa ameoka na kumletea Amnoni ndugu yake katika chumba cha kulala. 11 Alipomletea ili ale, Amnoni akamkamata kwa nguvu na kumwambia: “Njoo, ulale nami, dada yangu.” 12 Lakini Tamari akamwambia: “Usifanye hivyo ndugu yangu! Usiniabishe, kwa maana jambo kama hili halipaswi kufanywa katika Israeli.+ Usitende jambo hili la aibu.+ 13 Nitaondoaje aibu yangu? Nawe utaonwa kuwa kama mmojawapo wa wanaume wapumbavu katika Israeli. Sasa, tafadhali, ongea na mfalme, kwa maana hatakukataza unichukue.” 14 Lakini Amnoni akakataa kumsikiliza, akamzidi nguvu Tamari na kumwaibisha kwa kumbaka. 15 Kisha Amnoni akaanza kumchukia kwa chuki kali sana, hivi kwamba chuki hiyo ikawa kubwa sana kuliko upendo aliokuwa nao mwanzoni kumwelekea. Amnoni akamwambia: “Inuka; nenda zako!”
-