-
Yoshua 16:5-8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Na huu ndio mpaka wa wazao wa Efraimu kulingana na koo zao: Mpaka wa urithi wao upande wa mashariki ulikuwa Ataroth-adari,+ hadi Beth-horoni ya Juu,+ 6 na mpaka huo ulifika kwenye bahari. Mikmethathi+ ilikuwa upande wa kaskazini, na mpaka huo ulizunguka upande wa mashariki hadi Taanath-shilo, kuelekea upande wa mashariki hadi Yanoa. 7 Kisha ukashuka kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara na kupita Yeriko+ hadi Yordani. 8 Kutoka Tapua+ ukaelekea magharibi hadi kwenye Bonde la Kana, na kufika kwenye bahari.+ Huo ndio urithi wa kabila la Efraimu kulingana na koo zao;
-