-
Kutoka 1:19Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Wakunga hao wakamjibu Farao: “Wanawake Waebrania si kama wanawake Wamisri. Wana nguvu nao huzaa kabla mkunga hajafika.”
-
-
Yoshua 2:3-5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
3 Ndipo mfalme wa Yeriko akawatuma wajumbe kwa Rahabu, akisema: “Watoe nje wanaume waliokuja nyumbani mwako, kwa sababu wamekuja kuipeleleza nchi nzima.”
4 Lakini mwanamke huyo alikuwa amewaficha wanaume hao wawili. Basi akasema: “Ni kweli, wanaume hao walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka. 5 Giza lilipoingia, waliondoka kabla ya lango la jiji kufungwa. Sijui walikokwenda, mkiwafuatia haraka, mtawafikia.”
-
-
1 Samweli 19:12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Mara moja Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, ili akimbie na kutoroka.
-
-
1 Samweli 19:14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
14 Basi Sauli akawatuma wajumbe wamlete Daudi, lakini mke wa Daudi akawaambia: “Ni mgonjwa.”
-
-
1 Samweli 21:2Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
2 Daudi akamjibu kuhani Ahimeleki: “Mfalme aliniagiza nifanye jambo fulani, lakini akaniambia, ‘Usimjulishe mtu yeyote kazi niliyokutuma kufanya na maagizo niliyokupa.’ Nilikubaliana na vijana wangu tukutane mahali fulani.
-