5 Kisha mfalme akampa agizo hili Yoabu, Abishai, na Itai: “Mtendeeni kwa upole kijana Absalomu kwa ajili yangu.”+ Wanaume wote walimsikia mfalme akiwapa wakuu wote agizo hilo kuhusu Absalomu.
14 Ndipo Yoabu akasema: “Sitaendelea kupoteza muda pamoja nawe!” Basi akachukua mikuki mitatu midogo* na kumchoma nayo Absalomu kwenye moyo alipokuwa angali hai akining’inia kwenye mti mkubwa.