46 Kisha Musa akamwambia Haruni, “Chukua chetezo uweke moto ndani yake kutoka katika madhabahu+ na uweke uvumba juu yake, nawe uende haraka kwao na kuufukiza ili dhambi yao ifunikwe,+ kwa sababu Yehova amekasirika. Pigo limeanza!”
24 Yoabu mwana wa Seruya alikuwa ameanza kuwahesabu, lakini hakumaliza; hasira ya Mungu iliwaka dhidi ya Waisraeli kwa sababu ya jambo hilo,+ na idadi hiyo haikuandikwa katika masimulizi ya historia ya nyakati za Mfalme Daudi.