Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Mambo ya Nyakati 4:2-5
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 2 Alitengeneza Bahari*+ kwa madini yaliyoyeyushwa. Ilikuwa ya mviringo, yenye upana wa mikono 10 ukingo hadi ukingo na kimo cha mikono 5, na ingeweza kuzungukwa na kamba yenye urefu wa mikono 30.+ 3 Na chini yake kulikuwa na mapambo ya vibuyu,+ ambayo yalizunguka ukingo wote, vibuyu kumi kwa kila mkono mmoja kuzunguka Bahari yote. Vibuyu hivyo vilikuwa katika safu mbili, navyo vilitengenezwa kwa kuyeyushwa vikiwa sehemu ya Bahari hiyo. 4 Ilikuwa juu ya ng’ombe dume 12,+ watatu walitazama kaskazini, watatu walitazama magharibi, watatu walitazama kusini, na watatu walitazama mashariki; na Bahari hiyo ilikuwa juu yao, na sehemu zao zote za nyuma zilielekea katikati. 5 Na unene wake ulikuwa upana wa kiganja kimoja;* na ukingo wake ulitengenezwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi. Ingeweza kujaa maji kiasi cha bathi 3,000.*

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki