-
2 Samweli 8:10-12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Kwa hiyo Toi akamtuma Yoramu mwana wake kwa Mfalme Daudi ili amjulie hali na kumpongeza kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda (kwa maana mara nyingi Hadadezeri alimshambulia Toi); na Yoramu alimletea Daudi vitu vya fedha, dhahabu, na shaba. 11 Mfalme Daudi akavitakasa vitu hivyo ili viwe vya Yehova, pamoja na fedha na dhahabu aliyotakasa kutoka kwa mataifa yote aliyokuwa ameyashinda:+ 12 kutoka Siria na kutoka Moabu,+ kutoka kwa Waamoni, Wafilisti,+ Waamaleki,+ na kutoka katika nyara za Hadadezeri+ mwana wa Rehobu mfalme wa Soba.
-