Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Wafalme 10:16, 17
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 16 Mfalme Sulemani alitengeneza ngao kubwa 200 za dhahabu iliyochanganywa na madini mengine+ (kwa kila ngao alitumia shekeli 600* za dhahabu)+ 17 na ngao ndogo* 300 za dhahabu iliyochanganywa na madini mengine (kwa kila ngao ndogo alitumia mina tatu* za dhahabu). Kisha mfalme akaziweka katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni.+

  • 2 Mambo ya Nyakati 12:9-11
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Basi Mfalme Shishaki wa Misri akashambulia Yerusalemu. Akachukua hazina za nyumba ya Yehova+ na hazina za nyumba ya* mfalme. Alichukua kila kitu, kutia ndani ngao za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa ametengeneza.+ 10 Basi Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba zichukue mahali pa ngao hizo, akaziweka chini ya ulinzi wa mkuu wa walinzi,* aliyelinda mlango wa nyumba ya mfalme. 11 Wakati wowote ambapo mfalme alikuja katika nyumba ya Yehova, walinzi waliingia ndani na kuzichukua, kisha walizirudisha katika chumba cha walinzi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki