-
2 Mambo ya Nyakati 11:20-22Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 Kisha akamwoa Maaka mjukuu wa Absalomu.+ Baada ya muda akamzalia Abiya,+ Atai, Ziza, na Shelomithi. 21 Rehoboamu alimpenda zaidi Maaka mjukuu wa Absalomu kuliko wake zake wengine wote na masuria+ wake, kwa maana alikuwa na wake 18 na masuria 60, naye akawazaa wana 28 na mabinti 60. 22 Kwa hiyo Rehoboamu akamweka Abiya mwana wa Maaka kuwa mkuu na kiongozi miongoni mwa ndugu zake, kwa maana alikusudia kumweka kuwa mfalme.
-