53 Ndipo mwanamke fulani akaangusha jiwe la kusagia juu ya kichwa cha Abimeleki na kumpasua kichwa.+ 54 Abimeleki akamwita haraka mtumishi aliyembebea silaha na kumwambia, “Chomoa upanga wako uniue, watu wasije wakasema, ‘Mwanamke ndiye aliyemuua.’” Basi mtumishi wake akamchoma upanga, naye akafa.