-
2 Wafalme 9:24Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
24 Yehu akachukua upinde wake na kumpiga mshale Yehoramu katikati ya mabega, na mshale huo ukatokea moyoni mwake, naye akaanguka ndani ya gari lake la vita.
-
-
2 Wafalme 10:6, 7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
6 Ndipo Yehu akawaandikia barua ya pili, akisema: “Ikiwa mko upande wangu na mko tayari kunitii, leteni vichwa vya wana wa bwana wenu na mje kwangu kesho wakati kama huu kule Yezreeli.”
Wana 70 wa mfalme walikuwa pamoja na wanaume mashuhuri wa jiji waliokuwa wakiwalea. 7 Mara tu barua hiyo ilipowafikia, wakawachukua wana wa mfalme, wanaume 70,+ na kuwachinja, kisha wakaweka vichwa vyao ndani ya vikapu, wakampelekea kule Yezreeli.
-
-
2 Wafalme 10:25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Mara tu alipomaliza kutoa dhabihu ya kuteketezwa, Yehu akawaambia hivi walinzi* na makamanda wasaidizi: “Ingieni ndani na kuwaua! Msimwache yeyote aponyoke!”+ Basi walinzi na makamanda wasaidizi wakawaua kwa upanga na kuwatupa nje, wakaingia mpaka kwenye chumba kitakatifu cha ndani cha* nyumba hiyo ya Baali.
-