-
1 Wafalme 15:25-29Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Nadabu+ mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa Mfalme Asa wa Yuda, naye alitawala Israeli kwa miaka miwili. 26 Aliendelea kutenda maovu machoni pa Yehova na kufuata njia ya baba yake+ na dhambi yake aliyosababisha Waisraeli kutenda.+ 27 Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akapanga njama dhidi yake, na Baasha akamuua kule Gibethoni,+ jiji la Wafilisti, wakati Nadabu na Waisraeli wote walipokuwa wakilizingira Gibethoni. 28 Kwa hiyo Baasha akamuua katika mwaka wa tatu wa Mfalme Asa wa Yuda, akawa mfalme baada yake. 29 Mara tu alipokuwa mfalme, aliiangamiza nyumba yote ya Yeroboamu. Hakumwacha mtu yeyote wa Yeroboamu akipumua; aliagiza waangamizwe kama Yehova alivyokuwa amesema kupitia Ahiya, mtumishi wake kutoka Shilo.+
-