4 na Yezebeli+ alipokuwa akiwaua manabii wa Yehova, Obadia aliwachukua manabii 100 na kuwaficha katika mapango mawili, manabii 50 katika kila pango, naye alikuwa akiwapa mikate na maji.)
2 Ndipo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, akisema: “Miungu na iniadhibu, tena vikali, ikiwa kufikia kesho wakati kama huu sitakufanya uwe kama* kila mmoja wa manabii hao!”
15 Mara tu Yezebeli aliposikia kwamba Nabothi amepigwa mawe akafa, akamwambia Ahabu: “Inuka, chukua shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli,+ ambalo alikataa kukuuzia, kwa maana Nabothi hayuko hai tena. Amekufa.”