-
2 Mambo ya Nyakati 23:8-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
8 Walawi na watu wote wa Yuda wakafanya sawasawa na alivyoamuru kuhani Yehoyada. Basi kila mmoja wao akachukua wanaume wake waliokuwa na zamu siku ya Sabato, pamoja na wale ambao hawakuwa na zamu siku ya Sabato,+ kwa maana kuhani Yehoyada hakuwa ameviruhusu vikundi+ vilivyoshika zamu viondoke. 9 Kisha kuhani Yehoyada akawapa wakuu wa mamia+ mikuki na ngao ndogo* na ngao za mviringo zilizokuwa za Mfalme Daudi,+ ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mungu wa kweli.+ 10 Halafu akawaweka watu wote, kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi, kuanzia upande wa kulia wa nyumba mpaka upande wa kushoto wa nyumba, kando ya madhabahu na kando ya nyumba hiyo, kumzunguka mfalme pande zote. 11 Kisha wakamtoa nje mwana wa mfalme+ na kumvika taji na Ushahidi,*+ wakamweka kuwa mfalme, ndipo Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta. Halafu wakasema: “Mfalme na aishi muda mrefu!”+
-