-
2 Mambo ya Nyakati 23:12-15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Athalia aliposikia sauti ya watu wakikimbia na kumsifu mfalme, mara moja akaja na kujiunga na watu katika nyumba ya Yehova.+ 13 Kisha akamwona mfalme akiwa amesimama hapo karibu na nguzo ya mfalme karibu na lango. Wakuu+ na wapiga tarumbeta walikuwa na mfalme, na watu wote nchini walikuwa wakishangilia+ na kupiga tarumbeta, na waimbaji wakiwa na ala za muziki waliongoza katika kutoa sifa.* Ndipo Athalia akayararua mavazi yake na kupaza sauti: “Ni njama! Ni njama!” 14 Lakini kuhani Yehoyada akawatoa nje wakuu wa mamia, wale waliowekwa kulisimamia jeshi, akawaambia: “Mwondoeni miongoni mwa vikosi, na yeyote akimfuata, muueni kwa upanga!” Kwa maana kuhani alikuwa amesema: “Msimuue ndani ya nyumba ya Yehova.” 15 Basi wakamkamata, na alipofika njia ya kuingia katika Lango la Farasi la nyumba ya* mfalme, mara moja wakamuua hapo.
-