Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Mambo ya Nyakati 26:16-21
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 16 Hata hivyo, mara tu alipokuwa na nguvu, moyo wake ukawa na kiburi ambacho kilisababisha aangamie, naye alikosa kutenda kwa uaminifu kumwelekea Yehova Mungu wake kwa kuwa aliingia katika hekalu la Yehova ili kufukiza uvumba kwenye madhabahu ya uvumba.+ 17 Mara moja kuhani Azaria na makuhani wengine 80 wa Yehova wenye ujasiri wakamfuata humo. 18 Wakamkabili Mfalme Uzia na kumwambia: “Si vyema kwako, Uzia, kumfukizia Yehova uvumba!+ Ni makuhani tu wanaopaswa kufukiza uvumba, kwa maana wao ni wazao wa Haruni,+ waliotakaswa. Toka mahali patakatifu, kwa maana hujatenda kwa uaminifu, na kwa sababu hiyo hutapokea utukufu wowote kutoka kwa Yehova Mungu.”

      19 Lakini Uzia, aliyekuwa ameshika chetezo mkononi, akawaka hasira;+ na hasira yake ilipokuwa imewaka dhidi ya makuhani, ukoma+ ukatokea kwenye paji lake la uso mbele ya makuhani katika nyumba ya Yehova karibu na madhabahu ya uvumba. 20 Azaria mkuu wa makuhani na makuhani wote walipogeuka na kumtazama, waliona kwamba alikuwa amepigwa na ukoma kwenye paji la uso! Kwa hiyo wakamtoa humo haraka, naye mwenyewe akatoka nje haraka, kwa sababu Yehova alikuwa amemletea pigo.

      21 Mfalme Uzia aliendelea kuwa na ukoma mpaka siku aliyokufa, naye aliendelea kukaa katika nyumba iliyotengwa akiwa mtu mwenye ukoma,+ kwa sababu alizuiwa kuingia katika nyumba ya Yehova. Yothamu mwanawe ndiye aliyesimamia nyumba ya* mfalme, akiwahukumu watu nchini.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki