-
2 Wafalme 17:3-6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
3 Mfalme Shalmanesa wa Ashuru alipanda kuja kumshambulia,+ na Hoshea akawa mtumishi wake, akaanza kumlipa ushuru.+ 4 Hata hivyo, mfalme wa Ashuru alipata habari kwamba Hoshea alishiriki kupanga njama fulani, kwa maana alikuwa amewatuma wajumbe kwa Mfalme So wa Misri+ na hakuleta ushuru kwa mfalme wa Ashuru kama alivyofanya miaka iliyotangulia. Kwa hiyo, mfalme wa Ashuru akamfunga na kumtia gerezani.
5 Mfalme wa Ashuru aliivamia nchi nzima, naye akaja Samaria na kulizingira kwa miaka mitatu. 6 Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Hoshea, mfalme wa Ashuru aliliteka jiji la Samaria.+ Kisha akawapeleka Waisraeli uhamishoni+ kule Ashuru na kuwaweka katika eneo la Hala na Habori kando ya mto Gozani+ na katika majiji ya Wamedi ili waishi humo.+
-