-
2 Wafalme 18:9-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, yaani, mwaka wa saba wa Hoshea+ mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Mfalme Shalmanesa wa Ashuru alikuja kushambulia Samaria, akaanza kulizingira.+ 10 Nao wakaliteka+ baada ya miaka mitatu; Samaria lilitekwa katika mwaka wa sita wa utawala wa Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa utawala wa Mfalme Hoshea wa Israeli. 11 Kisha mfalme wa Ashuru akawapeleka Waisraeli uhamishoni+ kule Ashuru na kuwaweka katika eneo la Hala na Habori kando ya mto Gozani na katika majiji ya Wamedi ili waishi humo.+
-