-
Marko 8:6-8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
6 Naye akauagiza umati uketi chini. Kisha akachukua ile mikate saba, akatoa shukrani, akaimega, na kuanza kuwapa wanafunzi wake waigawe, nao wakaugawia umati.+ 7 Walikuwa pia na samaki wachache wadogo, naye akawabariki, kisha akawaambia wawagawe hao pia. 8 Basi wakala wakashiba, kisha wakakusanya vipande vilivyobaki wakajaza vikapu saba vikubwa.+
-
-
Yohana 2:7-9Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
7 Yesu akawaambia: “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza pomoni. 8 Akawaambia: “Choteni kidogo na kumpelekea msimamizi wa karamu.” Basi wakampelekea. 9 Msimamizi wa karamu alipoonja maji yaliyokuwa yamegeuzwa kuwa divai, bila kujua divai ilitoka wapi (lakini wahudumu waliokuwa wamechota maji hayo walijua), akamwita bwana harusi
-