-
Yeremia 41:1, 2Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
41 Katika mwezi wa saba, Ishmaeli+ mwana wa Nethania mwana wa Elishama, aliyekuwa wa uzao wa kifalme* na mmoja kati ya wakuu wa mfalme, akaja pamoja na wanaume wengine kumi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa.+ Walipokuwa wakila chakula pamoja huko Mispa, 2 Ishmaeli mwana wa Nethania na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye wakasimama na kumpiga kwa upanga Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani. Kwa hiyo akamuua mtu ambaye mfalme wa Babiloni alikuwa amemweka kuwa msimamizi nchini.
-