-
1 Samweli 27:8, 9Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
8 Daudi alikuwa akipanda pamoja na wanaume wake kuwavamia Wageshuri,+ Wagirzi, na Waamaleki,+ kwa maana walikuwa wakikaa katika nchi iliyoanzia Telamu mpaka Shuri+ na kushuka mpaka nchi ya Misri. 9 Daudi alipokuwa akiishambulia nchi, hakumwacha hai mwanamume wala mwanamke yeyote,+ bali alichukua kondoo, ng’ombe, punda, ngamia, na mavazi, kisha alirudi kwa Akishi.
-
-
1 Samweli 30:20Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 Basi Daudi akachukua makundi yote ya kondoo na ng’ombe, nao wakawatanguliza wanyama hao mbele ya mifugo yao wenyewe. Wakasema: “Hizi ni nyara za Daudi.”
-