Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Wafalme 22:13-17
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 13 Basi mjumbe aliyeenda kumwita Mikaya akamwambia: “Tazama! Manabii wote kwa pamoja wanasema mema kumhusu mfalme. Tafadhali, acha neno lako liwe kama maneno yao, useme mema.”+ 14 Lakini Mikaya akasema: “Kwa hakika kama Yehova anavyoishi, jambo lolote ambalo Yehova ataniambia ndilo nitakalosema.” 15 Kisha akaingia kwa mfalme, naye mfalme akamuuliza: “Mikaya, je, twende kupigana vita dhidi ya Ramothi-gileadi, au tusiende?” Mara moja akajibu: “Panda uende nawe utafanikiwa; Yehova atalitia jiji hilo mikononi mwako.” 16 Ndipo mfalme akamuuliza: “Nitakuapisha mara ngapi kwamba hupaswi kuniambia jambo lingine lolote isipokuwa ukweli katika jina la Yehova?” 17 Basi Mikaya akasema: “Ninawaona Waisraeli wote wakiwa wametawanyika milimani,+ kama kondoo wasio na mchungaji. Yehova akasema: ‘Hawa hawana bwana. Acha kila mmoja wao arudi kwa amani nyumbani kwake.’”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki