-
1 Wafalme 22:34, 35Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
34 Lakini mtu fulani alivuta upinde wake bila kukusudia na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya sehemu ambazo koti lake la vita linaungana. Basi mfalme akamwambia mtu aliyeendesha gari lake: “Geuka uniondoe vitani,* kwa sababu nimejeruhiwa vibaya.”+ 35 Vita vikapamba moto siku hiyo yote, nao wakalazimika kumsimamisha mfalme ndani ya gari akiwaelekea Wasiria. Damu ya jeraha lake ikamwagika ndani ya gari lake la vita, akafa jioni.+
-