41 Yehoshafati+ mwana wa Asa aliwekwa kuwa mfalme wa Yuda katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Ahabu wa Israeli. 42 Yehoshafati alikuwa na umri wa miaka 35 alipowekwa kuwa mfalme, naye alitawala kwa miaka 25 huko Yerusalemu. Mama yake aliitwa Azuba binti ya Shilhi.