-
2 Wafalme 11:1-3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
11 Basi Athalia+ mama ya Ahazia alipoona kwamba mwanawe amekufa,+ alitoka na kuangamiza uzao wote wa kifalme.*+ 2 Hata hivyo, Yehosheba binti ya Mfalme Yehoramu, dada ya Ahazia, akamchukua Yehoashi+ mwana wa Ahazia, akamwiba kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliopaswa kuuawa na kumweka yeye pamoja na mlezi wake katika chumba cha ndani cha kulala. Wakafanikiwa kumficha ili Athalia asimwone, kwa hiyo hakuuawa. 3 Akakaa pamoja naye kwa miaka sita akiwa amefichwa katika nyumba ya Yehova, Athalia alipokuwa akitawala nchi.
-