Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Wafalme 3:5-9
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 5 Huko Gibeoni, Yehova alimtokea Sulemani katika ndoto usiku na kumwambia: “Niombe unachotaka nikupe.”+ 6 Basi Sulemani akasema: “Umemtendea mtumishi wako Daudi baba yangu kwa upendo mwingi mshikamanifu alipokuwa akitembea mbele zako kwa uaminifu na kwa uadilifu na kwa unyoofu wa moyo. Umeendelea kumtendea kwa upendo huo mwingi mshikamanifu mpaka leo hii kwa kumpa mwana aketi kwenye kiti chake cha ufalme.+ 7 Na sasa, Yehova Mungu wangu, umeniweka mimi mtumishi wako niwe mfalme baada ya Daudi baba yangu, ingawa mimi ni kijana* tu na sina uzoefu.*+ 8 Mimi mtumishi wako ni miongoni mwa watu wako uliowachagua,+ watu wengi sana hivi kwamba hawawezi kuhesabiwa wala idadi yao kujulikana. 9 Basi nipe mimi mtumishi wako moyo mtiifu ili niwahukumu watu wako,+ nitofautishe mema na mabaya,+ kwa sababu ni nani anayeweza kuwahukumu watu hawa wako ambao ni wengi sana?”*

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki