12 Yehova akamwambia Abramu: “Ondoka katika nchi yako na kutoka kwa watu wako wa ukoo na nyumba ya baba yako uende katika nchi nitakayokuonyesha;+ 2 Nitakufanya kuwa taifa kubwa, nami nitakubariki, nami nitalifanya jina lako liwe kuu, nawe utakuwa baraka.+