-
Kutoka 23:10, 11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 “Kwa miaka sita utapanda mbegu katika shamba lako na kuvuna mazao yake.+ 11 Lakini mwaka wa saba hutalilima, utaliacha lipumzike, nao maskini walio miongoni mwa watu wako watapata chakula humo, na watakachoacha kitaliwa na wanyama wa mwituni. Hivyo ndivyo utakavyolifanyia shamba lako la mizabibu na shamba lako la mizeituni.
-
-
Mambo ya Walawi 25:4, 5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Lakini katika mwaka wa saba nchi itakuwa na pumziko kamili la sabato, sabato ya Yehova. Hampaswi kupanda mbegu wala kupunguza matawi ya mizabibu yenu. 5 Hampaswi kuvuna nafaka yoyote inayoota yenyewe baada ya mavuno, nanyi hampaswi kuchuma zabibu kutoka kwenye mizabibu yenu ambayo haijapunguzwa matawi. Ni lazima nchi iwe na mwaka wa pumziko kamili.
-