-
Esta 3:8-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
8 Kisha Hamani akamwambia Mfalme Ahasuero: “Kuna watu fulani waliotawanyika na kusambaa kati ya watu+ katika mikoa yote ya* milki yako,+ ambao sheria zao ni tofauti na za watu wengine wote, nao hawatii sheria za mfalme, na wakiachwa watamletea mfalme hasara. 9 Mfalme akipenda, amri ya kuwaangamiza Wayahudi na iandikwe. Nitawapa maofisa talanta 10,000 za fedha* ili waziweke katika hazina ya mfalme.”*
10 Ndipo mfalme akavua pete yake ya muhuri+ kutoka mkononi mwake, akampa Hamani+ mwana wa Hamedatha Mwagagi,+ aliyekuwa adui wa Wayahudi. 11 Mfalme akamwambia Hamani: “Umepewa fedha na pia watu hao ili uwatendee upendavyo.”
-