3 Kwa hiyo Yehova akawasikiliza Waisraeli na kuwatia Wakanaani mikononi mwao, Waisraeli wakawaangamiza pamoja na majiji yao. Basi wakapaita mahali hapo Horma.*+
5 Ndipo wafalme watano wa Waamori,+ yaani, mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi, na mfalme wa Egloni wakakusanyika pamoja na majeshi yao, wakaenda kupiga kambi ili kulishambulia jiji la Gibeoni.
10 Yehova akawavuruga,+ na Waisraeli wakawaangamiza wengi wao kule Gibeoni, wakawafuatia kwenye njia inayopanda kwenda Beth-horoni na kuwaua mpaka Azeka na Makeda.