-
Yoshua 24:12, 13Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Basi nikawafanya wavunjike moyo* kabla ya ninyi kufika, nao wakakimbia+—wafalme wawili wa Waamori. Hamkuwashinda kwa sababu ya upanga wenu wala upinde wenu.+ 13 Kwa hiyo niliwapa nchi ambayo hamkuipata kwa jasho lenu na majiji ambayo hamkujenga,+ nanyi mkakaa humo. Mnakula matunda ya mizabibu na ya mizeituni ambayo hamkupanda.’+
-
-
1 Wafalme 4:25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Watu wa Yuda na Israeli waliishi kwa usalama, kila mtu chini ya mzabibu wake mwenyewe na chini ya mtini wake mwenyewe, kuanzia Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.
-