23 Mwimbieni Yehova, dunia yote!
Tangazeni wokovu wake siku baada ya siku!+
24 Tangazeni utukufu wake miongoni mwa mataifa,
Kazi zake zinazostaajabisha miongoni mwa mataifa yote.
25 Kwa maana Yehova ni mkuu na anastahili kusifiwa kuliko wote.
Anaogopesha kuliko miungu mingine yote.+