-
Mwanzo 41:39-41Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
39 Kisha Farao akamwambia Yosefu: “Kwa kuwa Mungu amekuwezesha kuyajua yote hayo, hakuna yeyote aliye na busara na hekima kama wewe. 40 Wewe binafsi utaisimamia nyumba yangu, na watu wangu wote watakutii kabisa.+ Nitakuwa tu mkuu kuliko wewe ninapotimiza jukumu langu nikiwa mfalme.”* 41 Kisha Farao akamwambia Yosefu: “Tazama, ninakuweka kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri.”+
-
-
Mwanzo 41:48Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
48 Naye aliendelea kukusanya chakula chote cha miaka saba katika nchi ya Misri, akakiweka katika maghala majijini. Katika kila jiji alikusanya chakula kutoka katika mashamba yaliyozunguka jiji hilo.
-