-
Kutoka 8:6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
6 Basi Haruni akaunyoosha mkono wake juu ya maji ya Misri, na vyura wakaanza kuja na kuifunika nchi ya Misri.
-
-
Kutoka 10:12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Sasa Yehova akamwambia Musa: “Unyooshe mkono wako juu ya nchi ya Misri ili nzige waje juu ya nchi ya Misri na kula mimea yote nchini, kila kitu ambacho hakikuharibiwa na mvua ya mawe.”
-
-
Kutoka 10:21Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 Basi Yehova akamwambia Musa: “Unyooshe mkono wako kuelekea mbinguni ili giza liifunike nchi ya Misri, giza zito sana hivi kwamba linaweza kuguswa.”
-