Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Wafalme 1:16-21
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 16 Kisha Bath-sheba akainama na kumsujudia mfalme, mfalme akamuuliza: “Una ombi gani?” 17 Akajibu: “Bwana wangu, wewe ndiye uliyeniapia mimi kijakazi wako kwa jina la Yehova Mungu wako uliposema, ‘Sulemani mwana wako atakuwa mfalme baada yangu, na ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha ufalme.’+ 18 Lakini tazama! Adoniya amekuwa mfalme, na bwana wangu mfalme hujui lolote kuhusu jambo hilo.+ 19 Aliwatoa dhabihu ng’ombe dume, wanyama waliononeshwa, na kondoo wengi sana na kuwaalika wana wote wa mfalme na kuhani Abiathari na Yoabu mkuu wa jeshi;+ lakini hakumwalika Sulemani mtumishi wako.+ 20 Na sasa, bwana wangu mfalme, macho yote ya Waisraeli yanakutazama uwaambie ni nani atakayeketi kwenye kiti chako cha ufalme baada yako bwana wangu mfalme. 21 Usipofanya hivyo, mara tu utakapokufa na kuzikwa pamoja na mababu zako bwana wangu mfalme, mimi na mwanangu Sulemani tutaonwa kuwa wasaliti.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki