-
2 Samweli 15:32-34Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
32 Daudi alipofika kwenye kilele, mahali ambapo watu walizoea kumwinamia Mungu, Hushai+ Mwarki+ alikuwa mahali hapo ili kumpokea, joho lake lilikuwa limeraruka na alikuwa na mavumbi kichwani. 33 Hata hivyo, Daudi akamwambia: “Ukivuka kwenda pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu. 34 Lakini ukirudi jijini nawe umwambie Absalomu, ‘Mimi ni mtumishi wako, Ee mfalme. Nilikuwa mtumishi wa baba yako zamani, lakini sasa mimi ni mtumishi wako,’+ ndipo utakaponisaidia kuvuruga ushauri wa Ahithofeli.+
-