2 Kwa kuwa Yonathani mwana wa Sauli alimpenda sana Daudi,+ alimwambia hivi Daudi: “Sauli baba yangu anakusudia kukuua. Tafadhali jihadhari itakapofika asubuhi, nenda mahali pa siri na ujifiche huko.
4 Basi Yonathani akamsifu Daudi+ mbele ya Sauli baba yake. Akamwambia: “Mfalme, usimtendee dhambi mtumishi wako Daudi kwa sababu yeye hajakutendea dhambi na mambo aliyokufanyia yamekunufaisha.