-
Methali 23:29-35Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
29 Ni nani mwenye ole? Ni nani aliye na wasiwasi?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani anayelalamika?
Ni nani aliye na majeraha bila sababu? Ni nani aliye na macho mazito?*
31 Usiitazame rangi nyekundu ya divai
Inapong’aa katika kikombe na kushuka taratibu,
32 Kwa maana mwishowe huuma kama nyoka,
Nayo hutoa sumu kama nyoka kipiri.
34 Nawe utakuwa kama mtu anayelala katikati ya bahari,
Kama mtu anayelala juu ya mlingoti wa meli.
35 Utasema: “Wamenipiga, lakini sikuhisi chochote.*
Walinipiga, lakini sikujua.
Nitaamka lini?+
Nahitaji kinywaji kingine.”*
-