13 Baada ya siku chache, yule mwana mdogo akakusanya vitu vyake vyote akasafiri kwenda nchi ya mbali, akiwa huko akatumia vibaya mali yake kwa kuishi maisha ya anasa.* 14 Alipokuwa ametumia kila kitu, njaa kali sana ikatokea katika nchi hiyo yote, naye hakuwa na chochote.