Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Wafalme 21:8-11
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 8 Basi Yezebeli akaandika barua kwa jina la Ahabu, akazipiga muhuri wa Ahabu+ na kuzituma barua hizo kwa wazee+ na wakuu walioishi katika jiji la Nabothi. 9 Aliandika hivi katika barua hizo: “Tangazeni watu wafunge, halafu mketisheni Nabothi mbele ya watu. 10 Nanyi muwaketishe watu wawili wasiofaa kitu mbele yake ili watoe ushahidi dhidi yake,+ wakisema, ‘Umemtukana Mungu na mfalme!’+ Kisha mtoeni nje na kumuua kwa kumpiga mawe.”+

      11 Basi watu wa jiji lake, wazee na wakuu walioishi katika jiji lake, wakafanya kama ilivyoandikwa katika barua ambazo Yezebeli aliwatumia.

  • Yeremia 38:4, 5
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 4 Wakuu wakamwambia mfalme: “Tafadhali agiza mtu huyu auawe,+ kwa maana hivyo ndivyo anavyoidhoofisha mioyo* ya wanajeshi waliobaki jijini, na pia ya watu wote, kwa kuwaambia maneno hayo. Kwa maana mtu huyu hawatakii amani watu hawa, bali msiba.” 5 Mfalme Sedekia akajibu: “Tazama! Yuko mikononi mwenu, kwa maana mfalme hawezi kufanya jambo lolote ili kuwazuia.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki