5 Usinitazame,+
Ukinitazama nahangaika.
Nywele zako ni kama kundi la mbuzi
Linaloshuka kwenye miteremko ya Gileadi.+
6 Meno yako ni kama kundi la kondoo
Ambao wametoka kuoshwa,
Wote wamezaa mapacha,
Na hakuna yeyote aliyepoteza watoto wake.
7 Kama kipande cha komamanga
Ndivyo yalivyo mashavu yako nyuma ya shela yako.